HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Ukosefu wa bajeti watatiza mahakama tamba eneo bunge la Tiaty

Kuanzishwa kwa mahakama tamba katika kaunti ya Baringo miaka kumi iliyopita ilikuwa ni afueni kwa wakaazi wa eneo hilo waliokuwa wakitafuta haki kutokana na uhaba wa mahakama ambao uliwazimu hata kutembea mamia ya kilomita kufikia mahakama moja ya Kabarnet.
Lakini kutokana na kupunguzwa kwa bajeti ya mahakama, hali tete imetanda kwani sasa wakaazi wanalazimika kupata haki chini ya mti ambapo hakimu hujitokeza kusikiza na kuamua mamia ya kesi.

Show More

Related Articles