HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Mwangi Wa Iria apewa siku 14 kuwasilisha ripoti ya matumizi ya fedha

Kamati ya bunge la Senate kuhusu uhasibu imempa Gavana wa Murang’a siku kumi na nne kuhakikisha kwamba  afisi yake imetengeza ripoti dhabiti ya kujibu maswali ya ukaguzi.

Kamati hiyo aidha imemwambia gavana huyo kwamba ukosefu wa rekodi dhabiti pamoja na idadi inayofaa ya wafanyikazi vilichangia pakubwa katika kaunti hiyo kutotimiza malengo ya kukusanya ushuru.

Na huku akiunga mkono hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kusitisha miradi yoyote ya serikali hadi maswala ya kiuchunguzi yatatuliwe, Gavana wa Iria amekiri kwamba kumekuwa na changamoto kubwa kuwalipa waliokuwa wakihudumu chini ya serikali za wilaya japo kaunti yake imejaribu pakubwa.

Show More

Related Articles