HabariPilipili FmPilipili FM News

Visa Vya Ugaidi Vimetajwa Kupungua.

Visa vya kigaidi Kaunti ya Kwale vimetajwa kupungua kwa asilimia 60 chini ya kipindi cha miaka miwili hatua iliyotajwa kufanikishwa na ushirikiano  baina ya serikali na mashirika ya kijamii yanayoendeleza mpango wa kuhubiri amani katika jamii.

Kamishna wa Kaunti ya Kwale Karuku Ngumo amesema serikali ya kitaifa na ile ya kaunti zinashirikiana pamoja na wadau wote ili kuhakikisha visa vya kigaidi vinakabiliwa vilivyo katika jamii.

Aidha amedokeza kuwa serikali imeanzisha mpango wa kuwapeleka vijana katika vyuo vya kiufundi ili kuwawezesha kupata ujuzi wa kufanya kazi katika nyaja mbali mbali hatua inayolenga kuwaepusha na masuala ya kigaidi yanayotokana na misimamo mikali.

Ameongea haya baada ya kukutana na mashirika mbali mbali ya kijamii kujadili masuala ya misimamo mikali miongoni mwa vijana.

Show More

Related Articles