HabariPilipili FmPilipili FM News

Muungano Wa Wanahabari Nchini Walitaka Bunge Kutowashurutisha Wanahabari.

Baraza la wanahabri nchini limemtaka spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi kuondoa amri ya kuwataka wanahabari wawili wa gazeti la People Daily kufika mbele yake.

Hii ni baada ya wanahabari hao Dinah Ondari na Anthony Mwangi kuchapisha taarifa katika gazeti hilo iliyofichua bunge kuwa jumba la rushwa.

Baraza hilo limemtaka Muturi kuwasilisha suala hilo mbele yake kwa utatuzi.

Wakati huo huo katibu mkuu wa muungano wa wanahabari nchini KUJ Eric Oduor amelitaka bunge kukoma kuwashurutisha wanahabari.

 

Show More

Related Articles