HabariPilipili FmPilipili FM News

Mshukiwa Wa Wizi Auliwa Mombasa.

Mshukiwa mmoja wa wizi ameuwawa na polisi huku wawili wakibahatika kutoroka katika uwanja wa Cobla maeneo ya Mshomoroni kaunti ya Mombasa.

Akidhibitisha hayo OCPD wa kituo cha polisi cha Docks station Sangura Msee amesema mshukuwa huyo amepelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha Makadara huku akiomba vijana wajiepushe na uhalifu.

Aidha amewashukuru wananchi kwa ushirikiano wao huku akiwaomba uhusiano baina ya kitengo cha polisi na wananchi kizidi kuimarika.

Show More

Related Articles