HabariPilipili FmPilipili FM News

Wabunge Jumwa Na Dori Kuadhibiwa Na ODM

Chama cha ODM kimeanza kuonyesha makali yake kwa wabunge wawili wa chama hicho kutoka hapa Pwani ambao wanaaminiwa kuwa mahasimu wa chama hicho.

Wabunge hao Aisha Jumwa wa Malindi na Suleiman Dori wa Msambweni ambao waziwazi wameonyesha kumuunga mkono naibu rais William Ruto katika azma yake ya kuwania urais mwaka 2022,sasa huenda wakaadhibiwa na chama hatua ambayo huenda ikawapiga marufuku ndani ya chama hicho.

Sasa ODM imewapatia wawili hao siku saba kuelezea kwanini hawapaswi kuondolewa kwenye chama kwa uamuzi waliochukua.

Show More

Related Articles