HabariPilipili FmPilipili FM News

Wazazi Walaumiwa Kwa Ongezeko La Visa Vya Ubakaji Kilifi.

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Kilifi Gertrude Mbeyu amewalaumu wazazi  kwa ongezeko la visa vya ubakaji katika kaunti ya Kilifi.

Amesema visa vingi vya ubakaji vimekosa kuchukuliwa hatua mwafaka za kisheria kutokana na wazazi pamoja na maafisa tawala kuhujumu kesi hizo kwa kukataa kutoa na kuharibu ushahidi wa kesi hizo.

Naye mbunge wa Malindi Aisha Jumwa wakati wa uzinduzi wa muungano wa kina mama wa ‘KILIFI MUMS’ mjini Kilifi, aliyewanyoshea kidole cha lawama majaji humu nchini kwa ongezeko la visa vya ubakaji.

 

Show More

Related Articles