HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Ulanguzi wa watoto: Washukiwa 2 wakamatwa Mombasa akiwemo Daktari wa Singapore

Majasusi jijini Mombasa wamefichua kundi la wahalifu wakenya wanaoshirikiana na wengine kutoka Ughaibuni kuendeleza wizi wa watoto unaowalenga akina mama wanaobeba mimba na kujifungua watoto kwa niaba ya wenzao maarufu surrogate mothers.
Mwanamke mmoja Josephine Muthoni mwenye umri wa miaka 27 pamoja na mtaalamu wa afya Dkt. Mahesh Chudasama kutoka Singapore anayehudumu Mombasa, leo walitiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani  kufuatia tuhuma za kuiba watoto wachanga.
Mbele ya hakimu mkuu Henry Yyakweba, wawili hao walikanusha mashtaka ya wizi ya watoto kinyume na sheria ya mwaka 2004, kifungu cha nne ibara ya pili na tatu.
Dkt. Chudasama na Muthoni wanadaiwa kushirikiana kumkabidhi Neo Kian mtoto wa siku 12 ambaye walimbatiza jina Neo Yu Jie ili kufanikisha kusafirishwa kwa mtoto huyo hadi Singapore.

Show More

Related Articles