HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Waziri Amina awaeleza wabunge kwamba mwanafunzi wa Moi alidhulumiwa

Waziri wa Elimu Balozi Amina Mohamed sasa amedokeza kuwa ni bayana msichana wa kidato cha pili katika shule ya upili ya Moi girls hapa Nairobi alibakwa.
Akifika mbele ya kamati ya bunge kuhusu elimu, Amina amesema uchunguzi uliofanywa na madaktari kutoka hospitali mbili tofauti ulionyesha msichana huyo alitendewa uovu huo.
Hata hivyo Amina amewaelezea wabunge kwamba mikakati imo mbioni katika kukabiliana na visa vya uchomaji mabweni mbali na kuwataka washikadau kuwa katika mstari wa mbele kuhamasisha kuhusu athari za mwondoko huo.

Show More

Related Articles