HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Hukumu ya kifo yatathminiwa

Zaidi ya wafungwa 800 wanaokabiliwa na hukumu ya kifo huenda wakapata fursa ya kubadili kifungo chao na kuwa kifungo cha maisha gerezani.

Hii ni kufuatia mapendekezo yatakayowasilishwa na jopo kazi lililobuniwa kuangazia upya hukumu ya kifo.

Jaji Joseph Were anasema wameafikia vigezo vitakavyozingatiwa kwenye  rufaa hiyo ikiwemo umri wa mfungwa, hali ya kiafya kuambatana na uamuzi wa mahakama ya juu kwenye kesi iliyowasilishwa na Francis Morua Tetu.

Show More

Related Articles