HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wabunge waghadhabishwa na taarifa fichuzi kuhusu ufisadi

Gazeti la People Daily linalomikiwa na kampuni ya Mediamax limejipata kwenye mjadala wa bunge leo kufuatia taarifa za ufichuzi kuhusu ufisadi bungeni.
Kutokana na tetesi kutoka kwa wabunge spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi amewaagiza wanahabari wawili waliohusika ufichuzi huo kufika mbele ya kamati ya bunge ya mamlaka na fadhila bungeni alhamisi hii kufafanua taarifa hizo.
Hata hivyo katibu mkuu wa chama cha wanahabari nchini Erick Oduor ameshtumu bunge kwa kutoa mwelekeo huo anaoshikilia ni wa kupotosha.

Show More

Related Articles