HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Mwanasiasa Kurema Ole Surum arejesha hati miliki za ekari 175 Mau

Mwanasiasa mkongwe kutoka kaunti ya Narok sasa amerejesha hati miliki ya kipande cha ardhi alichomiliki ndani ya msitu wa Mau, kufuatia tishio la kuanzisha awamu ya pili ya kuwafurusha walowezi wote wanaoishi ndani ya msitu huo.

Kurema ole Surum ni mmoja wa watu mashuhuri waliotajwa kwenye ripoti ya aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga kuhusu mabwanyenye walionyakua msitu wa Mau na kuufanya mali binafsi.

Awamu ya pili ya kuwafurusha walowezi wa Mau itaanza wakati wowote kuanzia kesho na inalenga zaidi ya walowezi elfu arobaini.

Show More

Related Articles