HabariMilele FmSwahili

Idadi ya wasichana wanaopata mimba za mapema yaongezeka Mombasa

Idadi ya watoto wasichana wanaopata mimba za mapema imetajwa kuongezeka kwa kasi sana kaunti ya Mombasa. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na idara ya afya mwaka jana inaonyesha kuwa visa 3,000 vya wasichana walio chini ya umri wa miaka 18 waliotungwa mimba viliripotiwa katika zahanati mbali mbali za kaunti ya Mombasa. Afisa anayesimamia mpango huo Emmily Mwaringa amesema kuna zaidi ya visa 2,000 ambavyo havijaripotiwa na kuwataka wawakilishi wadi kubuni sheria ambazo zitalinda wasichana wadogo.

Show More

Related Articles