HabariMilele FmSwahili

Mvulana wa miaka 12 afikishwa mahakamani kwa kuwalawiti wanafunzi 5, Laikipia

Mvulana wa miaka 12 amefikishwa mahakama ya Nanyuki hivi leo kwa tuhma za kuwalawiti wanafunzi watano wa darasa la tatu shule ya msingi ya Temukis kijiji cha Ruai huko Laikipia.Moses Kariuki alifikishwa mbele ya hakimu wa Nanyuki Damacline Bosibori na kustakiwa kwa kosa hilo analodaiwa kutekeleza kati ya juni tarehe 16 na julai tarehe 23. Yadiawa aliwavizia wanafunzi hao waliokuwa wakicheza uwanja mmoja na kuwapeleka katika kichaka kilichokuwa karibu na kuwatendea unyama huo. Baadaye aliwatishia kwamba angeliwaua iwapo wangeelezea matukio yaliyowakuta. Hakimu huyo ameagiza mshukiwa kufanyiwa uchunguzi wam iaka yake na kurejehwa mahakamani tarehe 3 mwezi kesho.

Show More

Related Articles