HabariMilele FmSwahili

Majaji na Mahakimu wakosoa kupunguzwa bajeti ya mahakama

Chama cha majaji na mahakimu nchini kinadai uhuru wa idara ya mahakama huenda unahujumiwa kufuatiwa kupunguzwa bajeti inayotengewa idara hiyo kwa asilimia kubwa. Katika taarifa chama hicho kupitia katibu wake Derrick Kuto kimeshtumu bunge kufuatia hatua hiyo na huku akihofia kuathiriwa huduma muhimu za mahakama. Kuto ameomba serikali kuu kuingilia kati na kufadhili pesa zaiid kwa idara ya mahakama kufanikisha maeguzi ambayo yalikuwa tayair yameanza baada ya kuidhinishwa katiba mpya mwaka wa 2010.

Show More

Related Articles