HabariMilele FmSwahili

EACC yapendekeza polisi kuzuiwa kuendesha uchunguzi dhidi ya kesi za ufisadi

Tume ya ufisadi na maadili inapendekeza polisi kuzuiwa kuendesha uchunguzi dhidi ya kesi zinazohusu ufisadi na badala yake jukumu hilo kuachiwa makachero wa EACC pamoja na afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma. Naibu mwenyekiti wa tume hiyo Sophia Lepuchirit anatilia shaka maadili ya idara ya polisi na uwezo wao kuendesha uchunguzi huru. Anasema tume hiyo iwapo itapewa raslimali zaidi itakuwa na uwezo wa kutosha ikishirikiana na afisi ya DPP kuendesha uchunguzi na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa ufisadi.

Show More

Related Articles