People Daily

Mbunge wa Mwatate Andrew Mwadime Awataka Wafugaji Wasiotoka Kaunti Ya Taita Kufurushwa.

Baada ya kunaswa kwa simba kaunti ya Taita Taveta, sasa mbunge wa Mwatate Andrew Mwadime ametoa wito kwa wizara ya utalii nchini , kushirikiana na wizara husika kutoa mafunzo kwa wakaazi kuhusiana na mbinu za kuhifadhi nyasi ili kuwapa fursa ya kuziuza kwa wafugaji wanaosemekana kulisha mifugo ndani ya mbuga ya Tsavo.

Mwadime anasema  hatua hiyo itasaidia pakubwa wakazi kujiinua kiuchumi ikizingatiwa wafugaji hao wamekuwa wakiwalisha mifugo wao mbugani kwa ukosefu wa nyasi kwenye kaunti zao.

Aidha anatoa wito kwa wizara ya ufugaji kaunti hiyo kufanya msako na kuwafurusha mifugo wasiokuwa wa wenyeji wa kaunti hiyo , ambao huingia pasi kukaguliwa  kwani hali hii inahatarisha maisha ya mifugo ya wenyeji kuambukizwa magonjwa.

Show More

Related Articles