HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Kifo cha mwanafunzi chuoni Jomo Kenyatta chaibua maswali

Familia ya mwanafunzi wa miaka  22 wa chuo kikuu cha Jomo Kenyatta inamboleza kifo chake baada ya mwili wake kupatikana  katika kichaka eneo la Oasis Juja, kaunti ya Kiambu baada ya kuripotiwa kutoweka jumamosi wiki  iliyopita.

Tabitha Kitaa Kiiti alionekana mara ya mwisho baada ya kutoka densi na rafiki zake katika eneo la Juja siku ya jumatano.

Haya yanajiri huku biwi la simanzi likitanda katika kijiji cha Ingavila eneo bunge la Malava, Kakamega, baada ya kijana wa miaka 27 kumuua binamuye wa miaka 34 kwa kumdunga msumari wa nchi sita kifuani.

Show More

Related Articles