HabariMilele FmSwahili

Ochilo Ayacko kupeperusha bendera ya ODM kwenye uchaguzi wa useneta Migori

Ochilo Ayacko. ndiye atapeperusha bendera ya chama cha ODM kwenye uchaguzi wa useneta kaunti ya Migori. Mwenyekiti wa ODM John Mbadi anasema Ayako ambaye ni waziri wa zamani alikabidhiwa tiketi hiyo baada ya mchujo mkali ulioshirikisha wagombea wanane waliotaka tiketi ya ODM. Mbadi anasema walijadiliana na wagombea hao wote kabla ya kuafikia jina la Dr. Ochilo Ayacko.ambaye ana imani atamrithi mwendazake Ben Oluoch aliyefariki mwezi uliopita. Amewahakikishia wenyeji wa Migori hasa wafuasi wa ODM kwamba zoezi hilo lilifanywa kwa njia ya uwazi hivyo hakuna haja ya kuwa na wasi wasi ila kumchagua ayacko kuwawakilisha bungeni.

Show More

Related Articles