HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta kuongoza hafla ya kimataifa ya vijana mwezi Agosti kaunti ya Kisii

Rais Uhuru Kenyatta ataongoza hafla ya siku ya kimataifa ya vijana itakayoandaliwa kaunti ya Kisii mwezi Agosti. Rais anatarajiwa kutumia kongamano hilo kuwahimiza vijana kuhusu mbinu za kiweza kujitegemea. Aidha anatarajiwa kuzungumzia upandaji miti kwa minajili ya kuhifadhi mazingira na kuepusha athari za mabadiliko ya hali ya anga. Waziri wa jinsia na vijana profesa Margeret Kobia amedokeza kuwa maadhimosho ya mwaka huu yatakayoanza Agosti 6 hadi 12 pia yatatumika kuwahimiza vijana kuhusu mbinu za kushiriki katika utekelezaji wa ajenda nne kuu za rais Kenyatta na kuhubiri amani na mshikamano wa wakenya.

Show More

Related Articles