HabariPilipili FmPilipili FM News

Wananchi Waghadhabishwa Na Utendakazi Wamachifu Kilifi.

Zaidi ya wakaazi elfu moja wanaoishi katika Ranchi ya Kilifi huko Bamba wameelezea kutoridhishwa na utendakazi wa machifu na manaibu wao kwa kile wanachodai wamekuwa wakichukua fedha kutoka kwa jamii ya wasomali ili jamii hio iendelee na  shughuli ya kulisha mifugo yao katika sehemu hiyo.

Wakaazi hao wanadai jamii hiyo inamiliki zaidi ya Ng’ombe elfu 3 na Ngamia mia sita idadi ambayo wameitaja kuwa kubwa mno kuliko sehemu za malisho na huenda ikazua mtafaruku zaidi baina ya jamii hizo mbili ikiwa serikali haitaingilia kati swala hilo.

Wakiongozwa na Ramadhan Konde, wakazi hao wameitaka serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria maafisa hao kwani wamekuwa wakitumia vyeo vyao kujitafutua pesa.

Kwa upande wake mwanaharakati wa maswala ya kisiasa huko Bamba Daniel Mangi ameelezea kukerwa mno na hatua hio huku akizitaka taasisi husika humu nchini kuingilia kati swala hilo mara moja ili kudumisha amani kata ya jamii hizo.

Show More

Related Articles