HabariPilipili FmPilipili FM News

EACC Wakosoa Njia Yaukusanyaji Ushuru , Taita Taveta.

Tume ya kupambana na ufisadi nchini EACC tawi la pwani imekosoa serikali ya kaunti ya Taita Taveta, kuwaajiri wakusanyaji ushuru kama vibarua, ikisema hatua hiyo inachangia ufujaji wa pesa za umma.

Haya ni kwa mujibu wa kamishna wa tume hiyo Maalim Dabar, ambaye pia ameilaumu kaunti hiyo, kwa kutozingatia utumizi wa mfumo wa kiteknolojia wa usimamizi wa fedha IFMIS, na  badala yake kugeukia ule wa kizamani usiozingatia uwajibikaji.

Akitoa ripoti ya matumizi ya fedha ya mwaka wa 2015/2016, afisaa huyo pia amelikosoa bunge la kaunti hiyo kwa kukosa rekodi, ya shughuli za bunge la kaunti ikiwemo nakala za matumizi ya fedha.

Show More

Related Articles