HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Afisa wa IEBC amshtaki mwanawe na mpenziwe kwa wizi

Kulitokea sarakasi katika mahakama ya Milimani Nairobi baada ya msichana mmoja kuiambia mahakama kuwa mamake alikuwa amemshtaki mpenzi wake kwa kisingizio kuwa yeye alishirikiana na mpenziwe kumuibia shilingi  elfu sabini.
Msichana huyo anadai mamake alikerwa baada ya yeye kukataa kusitisha usuhuba wake na mpenziwe ambaye mamake anasema kuwa uume wake ni mdogo na hawezi kumtosheleza mwanaye kimapenzi.
Msichana huyo na mpenziwe walikuwa mbele ya Hakimu Mkuu  Francis Andayi  kwa mashtaka sita ya kuwa na nia ya kutekeleza uhalifu.

Show More

Related Articles