HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wazee elfu 40 waamua kuondoa ujinga kufuatia mikakati ya kaunti

Wazee wapatao elfu arobaini katika kuanti ya Pokot Magharibi, wameamua kujiunga na mfumo wa elimu kwa watu wazima almaarufu ngumbaru baada ya kaunti hiyo kuamua kuwapa elimu ya bila malipo.

Haya yanajiri kutokana na asilimia kubwa ya watu wasiojua kusoma na kuandika, katika eneo hilo.

Hata hivyo ni kibarua kwa walimu wao kwani wazee hao wakati wa mafunzo japo chini ya mti, huonekana kuendelea na shughuli zao bila  kutilia maanani walipo.

Show More

Related Articles