People Daily

Idadi Ya Wakenya Wanao Ugua Maradhi Ya Moyo Yaongezeka.

Kongamano la wataalamu wa magonjwa ya moyo limeng’oa nanga hapa Mombasa huku kauli mbiu ikiwa ni kueneza hamasa kuhusu ugonjwa huo.

Akizungumza katika kongamano hilo mkurugenzi wa muungano huo Naftali Omenta amesema wameshuhudia onegezeko la magonjwa ya moyo nchini huku akitaja mfumo wa maisha na ukosefu wa mazoezi kama sababu kuu zinazochangia ongezeko hilo.

Aidha amesema upungufu wa madaktari katika sekta hiyo ndio changamoto kubwa katika kupambana na magonjwa hayo.

 Vile vile rais wa muungano huo Bernard Gitura amesema ongezeko la msukumo wa damu mwilini ndio linasababisha magonjwa ya moyo.

Aidha amesema wanalenga kufanyia utafiti watu takribani 250,000 ili kudhibiti ongezeko hilo.

Show More

Related Articles