HabariPilipili FmPilipili FM News

Wahudumu Wa Afya Wanao Jihusisha Na Wizi Wa Dawa, Kwale Waonywa Vikali.

Kwa mara  nyingine  tena  naibu gavana wa Kwale Fatuma Achani amewaonya vikali wahudumu wa afya wanaojihusisha na visa vya  wizi wa dawa  katika hospitali za kaunti hiyo na kisha kuziuza katika maduka yao ya kibinafsi  ya kuuza dawa kuwa atakayepatika atakabiliwa kisheria.

Hii ni baada ya wakaazi  kulalamikia  uhaba mkubwa  wa dawa  katika hospitali kuu za kaunti,  huku wahudumu  wakiwaelekeza  kununua dawa hizo katika  maduka  ya dawa  wanayodaiwa  kuyamiliki.

Wakati uo huo amewataka wananchi kupiga ripoti iwapo watakumbana na hali zisizoeleweka katika hospitali hizo.

 

Show More

Related Articles