HabariMilele FmSwahili

Mahakama yaidhinisha ushindi wa mbunge wa Nyali Mohammed Ali

Mahakama ya rufaa mjini Mombasa imeidhinisha ushindi wa mbunge wa Nyali Mohammed Ali. Mahakama hiyo imetupilia mbali kesi iliyowasilishwa na mpiga kura Daniel Onyango Abwao. Mlalamishi huyo alidai kuwa uchaguzi ulikumbwa na hitilafu na kuwa ali alitumia picha ya kinara wa NASA Raila Odinga kwenye mabango yake ya kampeni licha ya kuwa mgombea huru kwenye uchaguzi wa Agosti nane.

Show More

Related Articles