HabariMilele FmSwahili

Shughuli za kusafirisha mafuta kutoka kaunti ya Turkana kurejelewa kesho

Huduma za usafirishaji mafuta kutoka kaunti ya turkana zinatarajiwa kurejelewa kesho serikali ikiahidi kupata mwafaka kuhusiana na lalama za wenyeji waliozuia shughuli hiyo. Katibu wa wizara ya petroli Andrew Kamau amesema waziri wa madini na petroli John Munyes anazuru Turkana leo kuongoza mikutano ya kutatua lalama za wenyeji ikiwemo utovu wa usalama. Anasema mkataba wa maelewano kutatua mgogoro huo utatiwa saini kesho.

Show More

Related Articles