HabariMilele FmSwahili

Mwanakemia wa serikali Ali Gakweli kufika mbele ya kamati ya bunge inayochunguza sakata ya sukari yenye sumu

Mwanakemia wa serikali Ali Gakweli leo anatarajiwa kufika mbele ya kamati ya pamoja ya bunge la taifa inayochunguza sakata ya sukari yenye madini ya sumu. Gakweli alikosa kufika mbele ya kamati hiyo jana hatua iliyoshutumiwa vikali na wabunge ambao pia walijibizana kuhusiana na watu wanaofaa kuhojiwa. Hali hii ilipelekea kamati hiyo kukosa kuwasilisha bungeni ripoti ya uchunguzi wake. Hata hivyo mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo Kanini Kega anasema Gakweli atahojiwa leo mchana

Show More

Related Articles