HabariPilipili FmPilipili FM News

Hatua Ya Serikali Kuunganisha Bandari Ya Mombasa Na Reli Ya Kisasa SGR Yapingwa Vikali.

Wawekezaji wa sekta ya uchukuzi wa mizigo kwa njia ya barabara wameeleza kuathirika pakubwa baada ya serikali  kutoa agizo la kuunganisha huduma za Bandari ya Mombasa na reli ya kisasa SGR

Mtaalam wa maswala ya kiuchumi David Ndii amesema agizo hilo limevunja sheria  kikatiba na kwamba huenda litaathiri pakubwa uchumi hapa Mombasa. Amesema usafirishaji wa mizigo kupitia reli ya SGR unagarimu  kiwango kikubwa cha pesa, licha ya kukosekana nafasi ya kubebea mizigo hiyo.

Kwa upande wake Gerald Kithi mmoja wanaopinga hatua hiyo ameitaka serikali kutamatisha kandarasi hiyo ya SGR kwa kuwa haifaidi mwananchi.

Vile vile William Odhiambo mtaalam wa kiuchumi amesema serikali haina haki kikatiba ya kugurisha huduma hizo, bali inafaa kuipatia serikali ya kaunti ya mombasa mamlaka ya kuendesha bandari ya KPA.

Show More

Related Articles