HabariMilele FmSwahili

Ruto ahidi kushauriana na bunge kuhusu bajeti ya idara ya mahakama

Naibu rais William Ruto ameahidi kushauriana na bunge kuhusu kupunguzwa bajeti ya idara ya mahakama. Ruto amemuhakikishia jaji mkuu David Maraga kwamba lalama za idara hiyo zitaashughulikiwa ili kutengewa raslimali za kutosha kutekeleza majukumu yao kikamilifu. Amesma ni lazima vitengo vyote vya serikali vipatiwe raslimali za kutosha kuendesha majukumu yao.

Kauli yake Ruto inawadia siku moja baada ya Maraga kulalama kwamba huduma muhimu za idara hiyo huenda zikasitishwa kufuatia mgao finyu ambao wametengewa na bunge. Ruto anasema hawataruhusu idara hiyo kufeli katika utendakazi wake.

Mahakama iliomba kutengewa shilingi bilioni 31 lakini ikatengewa bilioni 14.5 na bunge kwenye bajeti ya mwka huu wa kifedha wa 2018/19.

Show More

Related Articles