HabariPilipili FmPilipili FM News

Biashara Ya Peremende Yahofiwa Kusambaratika.

Inahofiwa kuwa huenda biashara ya utengenezaji wa peremende ikasambaratika baada ya serikali kuongeza ushuru wa asilimia 20 kwa kila kilo ya bidhaa hiyo.

Baadhi ya watengenezaji wa peremende hapa mombasa wakiongozwa na Roneek vora  wamesema sekta hiyo imepata hasara ya mamilioni ya pesa na huenda ikasambaratika kabisa iwapo serikali haitaingilia kati.

Wameitaka serikali kukuza wazalishaji wa humu inchini kwa kuondoa ushuru mkubwa unaowekewa bidhaa zao.

Kwa upande wake Mwalenga Mwagore amesema kampuni hizo zimeajiri jumla ya watu 3,479, na huenda watu hao wakapoteza kazi .

Aidha amesema ukosefu wa bidhaa ya sukari nchini na pingamizi katika kuipata bidhaa hiyo  umeathiri pakubwa sekta hiyo.

Show More

Related Articles