HabariMilele FmSwahili

Bunge la taifa kurejelea vikao vyake leo

Bunge la taifa linarejelea vikao leo, kibarua kikuu kinachowasubiri wabunge kikiwa kuwaidhinisha waliopendekeza na rais kusimamia tume mbalimbali zilizobuniwa kikatiba. Bunge litaangazia ripoti ya kamait iuliyompiga msasa Ben Chumo aliyependekezwa kuwa mwenyekiti wa tume ya mishahara. Chumo alifika mbele ya kamati ya fedha jana kuhojiwa ambako alijitetea dhidi ya ufisadi unaomkabili, haswa alipokuwa afisa mkuu mtendaji wa Kenya Power.

Pia bunge litaangazia uteuzi wa Florence Kajuju kama mwenyekiti wa tume ya haki. Mengine ambayo bugne itakabiliwa nayo ni pamoja na kuangazia ripoti ya kamati ya pamoja kuhusu biashara na kilimo iliyokuwa ikichunguza madai ya kuwepo sukari ya sumu nchini.

Show More

Related Articles