HabariPilipili FmPilipili FM News

Shirika La National Housing La Furusha Wakaazi Changamwe.

Vurugu Zimezuka katika nyumba za makazi ya National Housing huko Changamwe pale maafisa wa shirika hilo walipovamia  ploti nambari 416, iliyo na nyumba zaidi ya 30 na kuanza kuwafurusha wapangaji.

Baadhi ya wapangaji waliofurushwa wanasema  wameishi hapo kwa takriban miaka 30,   lakini wamekuwa wakiishi na hofu kubwa, baada ya  shirika la National Housing kuongeza kodi na kuapa kuwafurusha wote wenye madeni.

Baadhi yao wanasema wamepoteza vitu vya vya thamani katika zoezi hilo, wakisema maafisa wa shirika la National Housing wametumia vijana wahalifu kuwafurusha katika nyumba zao.

Show More

Related Articles