HabariPilipili FmPilipili FM News

Kilio Cha Wakaazi Taita Taveta.

Mamia ya wafugaji eneo la Mwatate kaunti ya Taita Taveta wameandamana hadi kwa ofisi ya kamishna ya kaunti ya Taita Taveta kulalamikia uvamizi wa simba katika makaaazi yao.

Wakaazi hao waliojawa na ghadhabu wamelisuta shirika la KWS kwa kushindwa kuwarudisha mbugani simba wanaondelea kuhangaisha wakaazi wa maeneo ya Chawia na Bura kwa wiki tatu mfululizo.

Kulingana nao Zaidi ya mifugo mia moja wameliwa na simba hao kufikia sasa,huku wakihofia kuwa huenda simba hao wakaanza kuvamia wakazi hususan watoto wanaorauka kwenda shule.

Show More

Related Articles