HabariPilipili FmPilipili FM News

Shirika La Msalaba Mwekundu Halikupewa Bilioni Moja Asema Waziri Matiang’i.

Waziri wa usalama wa ndani dkt Fred Matiangi amekanusha madai kuwa shirika la msalaba mwekundu lilipokea shilingi bilioni moja kutoka serikali kuongoza shughuli ya kuwapa makao mapya wahanga wa mkasa wa bwawa la Patel eneo la Solai.

Akifika mbele ya kamati ya seneti inayochunguza mkasa huo dkt Matiangi amesisitiza kuwa pesa zilizokabidhiwa shirika hilo zilikuwa za kuwafaa wahanga wa majanga ya mafurikko kote nchini.

Wakati huo huo Matiangi aameamuru uchunguzi ufanywe kuhusiana na wakuu wa wizara hiyo wamaodaiwa kupokea shilingi milioni 35 kuwalipa waathiriwa wa mkasa huo.

Matiangi ameahidi kuwasilisha ripoti kuhusiana na mkasa huo katika siku 30.

Show More

Related Articles