HabariMilele FmSwahili

Ubomoaji wa makaazi mtaani Kibera waendelea

Zoezi la ubomozi wa majengo katika mtaa wa Kibra linaendelea wakati huu. Mamlaka ya ujenzi wa bara bara kuu KENHA inaendesha zoezi hilo ili kuruhuru ujenzi wa bara bara itakayounganisha bara bara za Ngong na Langatta kupitia mtaa huo. Hata hivyo wakazi wamelalamikia kile wanakitaja kuwa zoezi hilo kuendeshwa kinyume na sheria wakidai serikali ilipaswa kuwapa makao mbadala kabla ya kuwafurusha. Hii ni licha ya kupokea agizo la mahakama kuondoka. jumla ya watu elfu 2o wataathirika na zoezi hilo.

Show More

Related Articles