HabariPilipili FmPilipili FM News

Hisia Mseto Zazuka Kuhusiana Na Kupakwa Kwa Rangi Ya Samawati Mombasa.

Agizo la kaunti ya Mombasa kuwataka wamiliki wa majumba yalioko katikati ya mji kuyapaka rangi majengo hayo linaendelea kuzua hisaia mseto.

Baadhi ya wakaazi wameonyesha kufurahia mabadiliko hayo , huku wengine wakiendelea kupinga uamuzi huo.

Wengi wanaishutumu serikali ya kaunti ya Mombasa chini ya uongozi wa Gavana Hassan Joho, kwa kuwashurutisha kupaka rangi ya samawati na nyeupe ambayo haiwapendezi.

Hatua ya mji kupakwa rangi inatokana na ilani iliyotolewa na serikali ya kaunti, kwa wakaazi na wamiliki wa majengo mnamo Machi mwaka huu 2018.

Show More

Related Articles