HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta aagiza kusitishwa utekelezaji wa miradi mipya ya serikali

Rais Uhuru Kenyatta ameagiza kusitishwa utekelezaji wa miradi mipya ya serikali. Rais amesema hakuna miradi mipya itakayozinduliwa hadi ile inayoendeshwa kwa sasa ikamilishwe. Akizungumza katika hafla iliyohudhuriwa na wakuu wa wizara na taasisi za serikali rais Kenyatta pia amesisitiza kuwa ukaguzi wa watumishi wote wa umma utaendelea ili kukomesha utumizi mbaya wa mamlaka na oporaji mali ya umma.

Show More

Related Articles