HabariMilele FmSwahili

Mbunge Gem Odhiambo apendekeza kurejeshwa adabu ya viboko shuleni

Mbunge wa Gem Elisha Odhiambo sasa anapendekeza kurejeshwa adhabu ya viboko shuleni kukabili utovu wa nidhamu. Odhiambo anasema wazazi wamerejea kuwabembeleza wanao hali anayosema matokeo yake ni uteketezaji shule unaoshuhudiwa nchini. Anasema iwapo adhabu hiyo itarejelewa huenda hali ilivyo kwa sasa nchini ikatulia. Kwa majuma 3 sasa zaidi ya shule 47 zimeteketezwa na wanafunzi na mali ya mamilioni ya fedha kuharibiwa kutokana na kile kimetajwa kama ukosefu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi

Show More

Related Articles