HabariMilele FmSwahili

Shirika la Amnesty International lapinga hukumu ya kifo iliyotolewa kwa Ruth Kamande

Shirika la Amnesty International limepinga hukumu ya kifo iliyotolewa kwa Ruth Kamande kwa kosa la kumuua mpenziwe Farid Mohammed.Amnesty International inataka hukumu hiyo kufutiliwa mbali na badala yake msichana huyo kuwekwa chini ya mpango wa kubadilishwa tabia. Katika ujumbe mkurugenzi wake Irungu Houghton anasema hukumu hiyo inakiuka haki yake ya maisha. Amnesty imeelezea masikitiko yake kuwa taifa linaendelea kutumia sheria hizo inazosema zimepitwa na wakati. Jaji Jessie Lesit alimpa hukumu akisema itatumika kama funzo kwa wengine walio na nia ya kuwaua wapenzi wao.

Show More

Related Articles