HabariMilele FmSwahili

Shughuli za ubomoaji katika ardhi yenye utata Arthi River zaendelea licha ya agizo la mahakama

Shughuli ya kubomoa makaazi na majengo kwenye ardhi yenye utata huko Athi River inaendelea licha ya wenyeji kupewa kibali cha mahakama kuzuia ubomoaji huo. Wenyeji wanazozania ardhi hiyo ya ekari 4000 inayodaiwa kumilikiwa na kampuni ya East African Portland. Wenyeji hao wanasisitiza kuwa hawataondoka kwenye ardhi hiyo ambako wamekuwa wa miongo kadhaa. OCPD wa sehemu hiyo Shama Wario ametakiwa kufika katika mahakma ya Machakos kutoa maelezo kuhusu ubomoaji huo.

Show More

Related Articles