HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wasiotambulika: Lydia Mumbua anasakata mpira akiwa na umri wa miaka 75

Ni mama mzee wa miaka 75, lakini yeye husakata mpira wa kandanda kiasi cha kuwaaibisha baadhi ya masogora wa soka.

Mama Lydia Mumbua huwatumbuiza wakazi wa mtaa wa Eastleigh hapa jijini Nairobi kila mara anapojitokeza na mpira na kucheza kwa ustadi nje ya nyumba yake.

Hii leo kwenye makala ya wasiotambulika, mama Lydia Mumbua anatuelezea jinsi amekuza kipawa chake hadi uzeeni na sasa anakitumia kuwapa changamoto vijana mtaani kuiga mfano wake wa kukuza vipawa.

Show More

Related Articles