HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

ANC yakatiza uwasilishaji wa mgao wa wabunge wake kwa NASA

Chama cha ANC sasa hakitakuwa kikiwasilisha hela ambazo wabunge wake wamekuwa wakikatwa kwenye mishahara kuchangia kapu la kuendesha shughuli za NASA.

Mbunge wa Lugari Ayub Savula ambaye pia ni mwenyekiti wa jopo la wabunge wa chama cha ANC amehakiki kuwa kulikuwa na mkutano wa wajumbe wa chama hicho na wamemuandikia karani wa bunge la kitaifa kwamba mgao waliokuwa wakitoa kwa muungano wa nasa usitishwe na badala yake hela hizo zielekezwa kwenye kapu la chama.

Show More

Related Articles