HabariPilipili FmPilipili FM News

COTU Yamkashifu Waziri Wa Fedha.

Shirika la  Kutetea  haki za wafanyikazi nchini COTU limemkashifu vikali waziri wa fedha Henry Rotich  kwa kupendekeza kodi kutolewa kutoka kwa marupurupu, na huduma za uhamisho wa fedha katika  bajeti ya 2018/2019.

Akiongea na wanahabari msaidizi  wa katibu mkuu  wa shirika hilo Ernest Nadome anasema kodi hizo zinakandamiza mwananchi wa kawaida na hivyo kuiomba serikali ya kitaifa kufanyia tathmini suala hilo.

Afisa huyo ametolea mfano njia mbadala za kuchangiza mapato ya taifa kama vile kupunguza idadi  ya wabunge na fedha za mgao wa kaunti.

Wakati huo huo amekashifu vikali wabunge waliosafiri Russia kuangalia michuoano ya kombe la dunia wakitumia mamilioni ya pesa za umma.

Show More

Related Articles