HabariPilipili FmPilipili FM News

Ethuro Aunga Mkono Juhudi Za Rais Kenyatta Za Kupambana Na Ufisadi.

Aliyekuwa spika katika bunge la seneti Ekwe Ethuro amesema migawanyiko inayoshuhudiwa baina ya kamati zilizowekwa kuchunguza kashfa mbali mbali za ufisadi nchini huenda ikalemaza juhudi za kupigana na janga la ufisadi.

Ethuro amesema ni jambo la kuhuzunisha kuona viongozi ambao wakenya wanawategemea wanalumbana badala ya kufanya kazi kwa pamoja na kuja na suluhuhisho kuhusiana na kashfa hizo.

Hata hivyo amesema anaridhishwa na hatua zinazochukuliwa na rais Uhuru Kenyatta na idara mbali mbali katika juhudi za kuhakikisha ufisadi unapigwa vita humu nchini.

Show More

Related Articles