HabariMilele FmSwahili

Wahudumu wa bodaboda watatiza shughuli za usafiri katika barabara ya University Way Nairobi

Shughuli za usafiri katika barabara ya University Way Nairobi zimetatizika baada ya wahudumu wa bodaboda kuandamana. Wahudumu hao wanalalamikia kugongwa kwa gari mwenyekiti wao. Wanadai gari lilimongonga linamilikiwa na kituo cha polisi cha Central. Ni ajali ambayo sasa wanahusisha na uhasama uliopo baina yao na serikali ya kaunti ya Nairobi kuhusu marufuku waliowekewa dhidi ya kuingia jijini Nairobi.

Show More

Related Articles