HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Makundi mawili yazozania usimamizi wa choo cha OTC-Nairobi

Sokomoko imeshuhudiwa mapema leo katika eneo la OTC hapa jijini Nairobi wakati maafisa wa polisi walipofika katika choo kimoja cha umma na kuwafurusha wafanyi kazi katika choo hicho huku wakiandamana na kundi la watu wanaodai kuwa wasimamizi halisi wa vyoo jijini.

Wakati huo huo, serikali ya kaunti ya Nairobi imekanusha madai kuwa ilihusika katika kisa hicho na kwamba itachukua usimamizi wa vyoo vya umma hapa jijini hivi karibuni.

Show More

Related Articles