HabariPilipili FmPilipili FM News

Shirika La Reli Kuongeza Idadi Ya Treni Za Kisasa.

Shirika la reli nchini KR linampango wa kuongeza idadi ya treni za SGR zinazosafirisha mizigo kutokea 7 hadi 12 kwa siku ifikapo mwezi desemba mwaka huu.

Kulingana na Meneja wa operesheni za shirika hilo Thomas Ojijo mpango huo utarahisisha kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo kutoka Bandari ya Mombasa hadi Nairobi,Ojijo pia ameongeza kuwa kiasi cha mizigo inayosafirishwa kimeongezeka kwa kiasi kikubwa tangu serikali ilipoingilia kati swala la utoaji vibali vya mizigo hiyo.

Aidha pia kulingana na Ojijo mabadiliko ya usimamizi katika bandari ya Mombasa Mabadiliko yataongeza  biashara. huku akisema SGR ilianza na treni 2   Februari mwaka huu na sasa imefikia treni 7.

Show More

Related Articles