HabariPilipili FmPilipili FM News

Vijana Wengi Pwani Hawana Vitambulisho.

TATIZO la vijana kukosa vitambulisho katika kaunti za pwani limeanza kuzua tumbo joto baada ya vijana wengi kukosa stakabadhi hiyo muhimu.

Uchunguzi wa msingi pia umebaini kuwa vijana wengi  hukosa ajira kwa kukosa vyeti vya kimasomo na hata vile vya kuzaliwa.

Mwanaharakati wa masuala ya jamii eneobunge la Jomvu Juma Athumani Lubambo sasa anapaza sauti kwa idara husika kuona kuwa suala hilo linashughulikiwa.

Kauli yake imeungwa mkono na chifu wa kata ya Chaani Ben Mutunga, akiwahimiza wazazi kupeleka watoto wao shuleni, ili waweze kuepukana na ukosefu wa ajira kwa kukosa stakabadhi muhimu.

Show More

Related Articles